27 October 2008

KANUNI ZA ULIMWENGU

SHERIA ZA ULIMWENGU
SHERIA YA UWEZEKANO:Uwezekano wa kutazamwa ni sawasawa na ujinga wa kitendo unachokifanya
SHERIA YA SIMU: Kila unapopiga wrong number lazima Simu ipokelewe
SHERIA YA UDHURU: Unapomwambia Bosi wako umechelewa kazini kwa sababu gari yako ilipata Pancha,siku inayofuata itapata Pancha
SHERIA YA FOLENI: Unapokimbilia Foleni nyingine,ile uliyoiacha itaanza kusogea haraka
SHERIA YA MAKUTANO: Uwezekano wa kuonwa na mtu anayekufahamu unaongezeka pale unapokuwa na mtu usiyetaka kuonekana naye
SHERIA YA MATOKEO: Unapotaka kumthibitishia mtu kwamba kifaa hakifanyi kazi, kitafanya
SHERIA YA SHUGHULI: Kwenye Shughuli yoyote,watu ambao Viti vyao viko mbali hufika mapema
SHERIA YA UBISHI: Kila kitu kinawezekana kama hujui unachokiongelea
SHERIA YA VIATU: Kiatu kikikutosha ni kibaya
SHERIA YA BIDHAA: Unapopata bidhaa unayoipenda,wanakuwa wameshaacha kuitengeneza
By sunbizo
bujI

No comments: