27 October 2008

WAZEE WA LIGI

Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi katiyao .Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi wa haja aliomfanyia mkewe ili wapime nani kabobea zaidi kwenye hiyo fani.
Mbishi 1 akasema: Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia mke wangu simu usiku kafungua simu hakusema haloo...kulaleki! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.
Mbishi 2 akatia: Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lakini hakusema karibu mume wangu...aliniangalia tu...nikaona analeta madharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.
Mbishi 3 akaunganisha: Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu tulipooana alikuwa anaona haya kunigusa...ananidengulia eti! na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.
Mbishi 1 na 2: Aaaaaaaah faza! acha usanii, nyie si mna watoto wawili lakini?
Mbishi 3: Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi... kwani mi nataka mchezo!.
Jamani wana ATSA,Ndani ya ATSA yetu nani anaweza kubishana na hawa jamaa?

Jibu kwa sunbizo
Buji.

No comments: